Genesis 5:28-32

28Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana. 29 aAkamwita jina lake Nuhu, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Bwana.” 30Baada ya Nuhu kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 31Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa.

32 bBaada ya Nuhu kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.
Copyright information for SwhKC